Simba SC itacheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi B wa CAF Champions League dhidi ya Jwaneng Galaxy siku ya Jumamosi ya March 02, 2024 katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Kuelekea mchezo huo Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally ametangaza kuwa siku hiyo Mgeni rasmi atakuwa Inonga Baka.

“Mgeni rasmi ni Inonga Baka tumeamua kumpa heshima hii kwa sababu ndio Mchezaji pekee ambaye ameipeleka timu yake ya Taifa (Congo) nafasi ya nne kwenye AFCON, kwenye mechi dhidi ya Jwaneng yeye ndio Mchezaji pekee aliyeipeleka timu yake nafasi ya nne”

Huo ni mchezo muhimu kwa Simba SC kushinda ili kwenda robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement