"Ahsante sana kwa mchango wako ndani ya klabu yetu ukiwa kama nahodha, kocha msaidizi. Ulikuja Azam FC ukiwa mdogo sana mwaka 2009 kama mchezaji hadi leo unaondoka ukiwa sehemu ya benchi letu la ufundi," imesema taarifa ya Azam FC mapema leo.

Huyo anakuwa mtu wa nne kuondolewa katika benchi la Ufundi baada aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu Kali Ongala, Kocha wa Makipa, Mspaniola Dani Cadena na kocha wa Fiziki, Mtunisia Dk. Moadh Hiraoui.


Makocha hao wanaondoka kupisha wasaidizi wapya watakaoletwa na kocha mpya, Msenegal Youssouph Dabo ambaye ataanza kukiandaa kikosi kwa ajili ya msimu ujao.


Tayari Azam FC imeachana na wachezaji watano, ambao ni beki Mzimbabwe Bruce Kangwa, kiungo Mkenya, Kenneth Muguna na mshambuliaji Mzambia, Rodgers Kola na wazawa Ismail Aziz na Cleophace Mkandala.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement