Suala la afya ya Mohamed Salah limeibua mvutano kati ya Chama cha Soka cha Misri (EFA) na Klabu ya Liverpool ambapo kila upande unavuta upande wake ukiona una haki ya kumtumia na kujua maendeleo ya majeraha yake. 

Liverpool imedai hajakaa sawa tangu alipoumia Januari 2024 aliposhiriki AFCON, hivyo imeandika barua kwenda EFA kuomba Salah kutojumuishwa katika Kikosi cha Timu ya Taifa ya Misri inayotarajiwa kuweka kambi Abu Dhabi kwa ajili ya Mechi za Kirafiki lakini EFA imeweka jina la Mchezaji huyo katika orodha ya Wachezaji wanaotakiwa kuingia kambini. 

Tangu atoke AFCON, Salah amecheza mechi moja, pia Liverpool inataka kumtumi mechi ijayo dhidi ya Manchester City, Machi 10, 2024 kisha apewe muda wa kupumzika. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement