Afrika inatarajia kuandaa Michezo ya Olimpiki ya Vijana kwa mwaka 2026 ikiwa ni kwa mara ya kwanza kabisa kuandaliwa barani humu.

Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) Thomas Bach ameeleza kuwa michezo hiyo itakafyika Dakar, mji mkuu wa Senegal na imeratibiwa upya kufanyika kati ya Oktoba 31 na Novemba 13 mwaka 2026 ambapo hafla hiyo inayopendekezwa inatazamiwa kuwaleta pamoja wanamichezo bora zaidi duniani ili kushindana katika michezo 35 tofauti kwa muda wa siku 14.


Thomas Bach anaripotiwa kuunga mkono uandaaji wa Michezo ya Olimpiki ya Vijana ya Senegal, akibainisha umoja wa Afrika na utamaduni wake wa kimichezo ambapo aliweka wazi kuwa Pamoja na idadi ya vijana na mapenzi ya michezo lakini kwa sasa ni wakati wa Afrika na niwakatiwa Senegal.

Bach aliweka wazi kuwa Kuandaliwa kwa Michezo ya Olimpiki ya Vijana huko Dakar kunawakilisha hatua kubwa katika kuonyesha vipaji na uwezo wa wanamichezo wachanga kwenye jukwaa la kimataifa.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement