Shabiki wa Ivory Coast aitwaye Anselme Santos, ameomba radhi hadharani kwa Mkewe, Watoto baada ya video zake kusambaa akonekana kwenye TV anamuomba namba ya simu Mwanamke ambaye ni Shabiki wa Senegal.

“Katika ile video nilionekana kumuomba namba ya simu, sikuwa namaanisha lakini pia hakutaka kunipa, ningependa kutumia fursa hii kuomba radhi kwa Mke wangu na Watoto wangu”

Mitandao ya Ivory Coast imeripoti kuwa Tukio hili la Santos lilitokea wakati wakiwa uwanja kwenye mechi ya 16 bora katika mashindano ya AFCON 2023 ambapo Ivory Coast ilikua ikicheza dhidi ya Senegal ambapo Ivory Coast walivuka kuingia hatua ya robo fainali kwa kuwatoa Senegal kwa penati 5-4. 

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement