Abdjan Ivory Coast. Kocha wa DR Congo, Sebastien Desabre amesema anaamini sasa wana nafasi nzuri zaidi ya kutwaa ubingwa wa Mataifa ya Afrika baada ya kufika nusu fainali,huku akiwataja mastaa wake.

DR Congo inayoundwa na wakali kibao akiwamo beki wa Simba, Henock Inonga Baka, iliifunga Guinea mabao 3-1 Ijumaa na kutinga nusu fainali ya Afcon 2023 ambako sasa itakutana na wenyeji Ivory Coast kesho.

Timu hizo mbili zitakutana kwenye Uwanja wa Olympique Alassane Ouattara, huku DRC mara ya mwisho kutwaa taji la Afcon ikiwa mwaka 1974.

Wenyeji Ivory Coast walitwaa taji hilo mara ya mwisho mwaka 2015 nawame dhamiria kulibeba tena mbele ya mashabiki wao pamoja na kuanza vibaya kwenye michuano ya mwaka.

Kocha huyo amesema anawategemea mastaa wake watampa ushindi kwenye mchezo wa kesho, pamoja na ule wafainali ambao anaamini watacheza,huku akiwataja Inonga na mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Fiston Mayele kama silaha zake.

"Itakuwa ni ujinga kuacha kuamini kwamba tutashinda fainali. Lakini itakuwa ni ngumu. Tuna washambuliaji kama (Cedric) Bakambu, (Simon) Banzana Mayele Fiston. Tunajua kwamba niishu ya muda tu kabla hatujatwaa ubingwa.

"Unapofika nusu fainali, jambo la kwanza unataka kufika fainali na kama ukiweza kufika fainali, unataka kushinda ubingwa. Tutafanya kila kitu kutwaa ubingwa huu kwa kuwa tunasafu mzuri ya ulinzi inayoongozwa na mabeki wazoefu, wenye uwezo najuhudi, yupo Inonga, Masuaku Arthurtuna kipa bora kama Mpasi Lionel na kikosi kizima, hatuna cha kujutia."

Kabla ya kukabiliana na Guinea, Chuiwa Congo walitoka sare tatu katika hatua ya makundi 1-1 dhidi ya Zambia,1-1 dhidi ya Morocco na 0-0 dhidi ya Taifa Stars ya Tanzania.

Kwenye hatua ya 16-Bora, pia DR Congo ilitoka sare ya 1-1 dhidi ya mabingwa wakihistoria wa michuano hiyo, Misri kabla ya kuwaondoa Mafarao hao kwa penalti 8-7.

Wacongo walianza kuwa watamu katika hatua ya robo fainali ambako waliichakaza Guinea 3-1.

"Ubora huu umekuja muda mwafaka wakati tunalikaribia kombe" alisema kocha Desabre wakati akijiandaa kuivaa Ivory Coast katika nusu fainali kesho Wakati kocha huyo akizitaja silaha zake hizo, inaonekana Inonga ni mchezaji muhimu zaidi kwenye kikosi chake,akiwa amecheza dakika 315 kwenye michuano ya Afcon msimu huu, lakini kwa Mayele ambaye alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kuisaidia nchi yake kabla ya michuano hii, hajapata nafasi kubwa akiwa ametumika kwenye dakika 106 tu.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement