AFCON: MCHEZO WA TAIFA STARS NA DR CONGO KUPIGWA MWAKANI
sasa akili ya Taifa Stars ni Fainali za Africa (Afcon) nchini Ivory Coast kuanzia Januari 13 na kuhitimishwa Februari 11.
Usiku wa kuamkia leo, Stars ilikivwasha na Morocco kwenye mchezo wa pili wa kufuzu kombe la Dunia 2026 na Stars imekubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa wageni wao katika Uwanja Lakini Stars watakutana tena na Morocco kwenye mechi yao ufunguzi ya Afcon Januari 17, saa 2 usiku. Katika
fainali hizo, Stars imepangwa kundi 'F itaanza kampeni zake kwa kucheza na Morocco lakini baada ya hapo watakiwasha na Zambia Januari 21.
Mechi nyingine kwenye fainali hizo itakuwa dhidi ya DR Congo Januari 24. Licha ya Stars kubeba matumaini makubwa kwa mashabiki nchini, jambo kubwa ambalo kocha mkuu, Adel Amrouche ana kazi ya kufanya ni kuboresha eneo la ushambuliaji ambalo bado halijawa na makali ya kuridhisha licha ya kwamba amesisitiza kuibuka na mipango mipya.
Stars imekuwa na mastaa wanaocheza nje na kuongeza ushindani kama ilivyotokea kwenye mchezo na Niger ambapo, Charles MMombwa aliyefunga bao la ushindi alionyesha kiwango bora.
Nyota huyo anayeichezea klabu ya Macarthur ya nchini Australia licha ya kujumuishwa kwa mara ya kwanza na alionyesha ubora.