AFCON 2027: UWANJA MPYA WA SOKA WA NAKIVUBO, KAMPALA UGANDA
Rais wa Uganda Yoweri Museveni amefungua uwanja huo rasmi, baada ya shughuli za ujenzi zilizoanza 2017 kumalizika.
Uwanja wa Nakivubo unatarajiwa kuwa na mchango mkubwa kwenye maandalizi ya Uganda ya Kombe la Afcon 2027 ambapo itakuwa mwenyeji pamoja na Kenya na Tanzania.
Ukarabati wa Uwanja huo ulitekelezwa na mfanyabiashara Hamis Kiggundu chini ya mpango wa Ushirikiano wa sekta za Umma na Binafsi.
Mfanyabiashara huyo Kiggundu amepewa kandarasi ya kusimamia uwanja huo kwa miaka 49.