AFCON 2027: TADHIMINI IMESHAKAMILIKA NA SASA TUPO KWENYE MAPATANO
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo, Ally Mayay amesema waandaaji wa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027; Tanzania, Kenya na Uganda kila nchi itapaswa kuwa na viwanja vitatu na kwamba Tanzania tayari inavyo viwili Benjamin Mkapa na Amaan Zanzibar hivyo umebaki uwanja mmoja ambao utajengwa Arusha.
Mayay amesema mambo ya tathimini yalishakamilika na sasa wako katika hatua ya mapatano, na kwamba ujenzi wa uwanja huo mpya wenye uwezo wa kubeba watu 30,000 utaanza kujengwa mwezi ujao.
“Tuko kwenye hatua za mwisho na mkandarasi wa ujenzi wa uwanja wa Arusha, mpaka Desemba 2025 CAF watakuja kuangalia tayari utakuwa umekamilika.”