Wachezaji wa DR Congo wote walishika mikono yao ya kulia mbele ya vinywa vyao na vidole viwili kwenye vichwa vyao huku wakitumia nafasi yao katika Kombe la Afcon kuitisha uangalizi wa kimataifa kwa minajili ya kuleta amani katika eneo lenye machafuko la mashariki mwa nchi yao.

Hii ni baada ya Shirikisho la Soka barani CAF kuiruhusu DRC wakiwemo wachezaji kuvaa utepe mweusi mikononi kama “ishara ya maombolezo” na “mshikamano” na waathiriwa wa mzozo huo.

Nyota wa DRC wamesifika kwa kutumia jukwaa hilo kuyataka mataifa kuangazia mzozo uliosahaulika na ghasia za silaha zinazoendelea mashariki mwa nchi yao.

“Ulikuwa ujumbe kuonyesha msaada kwa waathirika, kuwajulisha (watu) kwamba kuna ukweli mambo yanayotokea katika mashariki na kwamba ni muhimu kutoa mwanga juu yake. Watu wamevunjika moyo juu ya hilo, pia, ” Kocha Sebastien Desabre alisema baada ya timu yake kupoteza 1-0.

DRC imemaliza katika nafasi ya 4 kwenye Kombe la Afcon 2023.

You Might Also Like

Get Newsletter

Advertisement