ADEMOLA LOOKMAN AIPA UBINGWA WA EUROPA ATALANTA KWA KUIFUNGA HAT-TRICK BAYER LEVERKUSEN
Ademola Lookman alijiingiza katika rekodi za Atalanta kwa kufunga hat-trick katika Fainali ya Ligi ya Europa na kuipa timu yake Ubingwa wa Michuano hiyo ameweka wazi kuwa haikumshangaza ingawa kocha Gian Piero Gasperini amekiri kuwa hakuna ambaye alitarajia.
Winga huyo wa Nigeria mzaliwa wa London amekuwa mchezaji wa sita kufunga hat-trick katika fainali ya Uropa - ya kwanza tangu Jupp Heynckes kuichezea Borussia Monchengladbach kwenye Kombe la Uefa mwaka 1975 akiwa na mabao yote matatu katika ushindi wa timu ya Italia dhidi ya Bayer Leverkusen huko Dublin.
Kwa upande wake Kocha wa Atalanta Gasperini amesema amepata kitu ambacho kitasalia katika kumbukumbu za historia ya soka.
Ingawa hii inaweza kukumbukwa kama fainali ya Lookman, mafanikio ya Atalanta ni ya kushangaza vile vile ambapo Katika historia yao ya miaka 116, hili linakuwa taji lao la pili - baada ya Coppa Italia ya mwaka 1963 ambapo wiki iliyopita tu walipoteza fainali ya Coppa Italia kwa Juventus.
Vijana wa Gasperini pia wanakuwa timu ya kwanza ya Italia kushinda mashindano haya tangu mwaka 1999.